Rais John Pombe Magufuli wa Tanzania amefariki dunia. Alikuwa na umri wa miaka 61 mauti yalipomkuta tarehe 17 Machi mwaka huu wa 2021 katika hospitali ya Mzena jijini Dar es salaam nchini humo alikokumbwa amelazwa akisumbuliwa na maradhi ya moyo. Tayari taifa hilo la Afrika Mashariki limeanza maombolezo ya siku 14 huku bendera zikipepea nusu mlingoni.
0 Comments