HISTORIA YA RAIS SAMWEL KANYON DOE




Huyu ndiye SAMUEL KANYON DOE rais aliyeuawa kikatili sana nchinii Liberia,,,, Samuel Kanyon Doe alizaliwa May 6, 1951 jijini Tuzon, nchini Liberia. Alfajiri ya Aprili 12, 1980, kikundi kidogo cha wanajeshi 17 kilijipenyeza ndani ya makazi ya Rais jijini Monrovia... Ikulu walimkuta Rais William Tolbert bado amelala... Wakamuua. Aliyeongoza kikundi hicho alikuwa askari kijana na wa cheo cha chini, Sajenti Samuel Doe. Na inasemwa kuwa Doe alipoingia Ikulu na wenzake, alidhani watakwenda kumlalamikia Rais juu ya mishahara midogo ya askari wa vyeo vya chini... Lakini jinsi walivyoikuta Ikulu ikiwa nyepesi vile, ndivyo mipango ilipobadilika na kuamua kumuua Rais mwenyewe na kuchukua madaraka. Samuel Doe alikuwa askari ambaye hata madarasa manne ya shule ya msingi hakuyamaliza... Alitoka kabila dogo la waishio misituni, kabila la Krahn... Ni watu wa kabila kama lake, masikini na ambao ndio waliotoka vijijini na kukimbilia jijini Monrovia kutafuta vibarua na pesa. Kwa wenye bahati, kama Samuel Doe, walionekana mitaani na kuitwa kujiunga na Jeshi. Na kama ilivyokuwa kwa Idi Amin, Urais ulimdondokea tu Samuel Doe, kama vile mtu aliyeshinda bahati nasibu... Ujio wa Samuel Doe uliwafaya WaLiberia waamini kuwepo kwa mabadiliko... Kuondokana na utawala wa kifisadi na kirasimu wa William Tolbert. Samuel Doe akajitangaza kuwa Rais, April 12, 1980... Haraka sana akawatwanga risasi mawaziri wote wa Tollbert... Ni kwenye pwani ya bahari huku wananchi wakitazama kama mechi ya mpira... Sajenti Samuel Doe akatawala kwa kipindi cha miaka kumi... Nchi ikawa kama imesimama. Watu wa kabila la Samuel Doe waliogopewa na makabila mengine… Waliweza kufanya lolote lile na hakuna aliyewagusa… Waliua na waliwatisha wengine... Wengi wasio wa kabila la Rais Doe, waliishi kwa hofu kubwa… Na kile ambacho kila mtu asiye wa kabila la Doe, alikuwa anakisubiri, ni kushuhudia mwisho wa Sajenti Samuel Doe. Ndipo hapa akatokea Charles Taylor… Huyu alikuwa rafiki wa zamani wa Sajenti Samuel Doe. Lakini, urafiki wao ulikufa pale Samuel Doe alipodai kuwa Charles Taylor alimtapeli dola milioni moja… Kisha Taylor akatorokea Marekani… Huko akaanza kufanya biashara kwa mtaji wa fedha alizomtapeli Sajenti Samuel Doe. Charles Taylor naye akaishia gerezani nchini Marekani kwa mashtaka ya utapeli… Lakini akatoroka jela na kukimbilia Ivory Coast... Na akiwa Ivory Coast, Charles Taylor akaanza kujipanga kwenda kuuangusha utawala wa Sajenti Samuel Doe… Charles Taylor akiwa Ivory Coast, alikiandaa kikosi cha,,,,,,,,!!! WAPENDWA, STORY INAENDELEA KWENYE GROUP. WEKA NAMBA YAKO TUKUUNGE KWENYE GROUP LETU LA STORIES ZA KUSTAAJABISHA ILI UWEZE KUIMALIZIA STORY HII PAMOJA NA KUJIPATIA STORIES NYINGI ZAIDI ZA KUSTAAJABISHA. MPENDWA, PIA USISAHAU KUBOFYA LINK HIYO HAPO CHINI, HAKIKA UTASTAAJABIKA KWA UTAKACHOKIONA . #SAMWELDOE